Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 40

Faatir 35:40

فاطر

قُلْ أَرَءَيْتُمْ شُرَكَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَرُونِى مَاذَا خَلَقُوا۟ مِنَ ٱلْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ أَمْ ءَاتَيْنَـٰهُمْ كِتَـٰبًا فَهُمْ عَلَىٰ بَيِّنَتٍ مِّنْهُ ۚ بَلْ إِن يَعِدُ ٱلظَّـٰلِمُونَ بَعْضُهُم بَعْضًا إِلَّا غُرُورًا

Maana

Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba sehemu gani katika ardhi? Au wana ushirika wowote katika mbingu? Au tumewapa Kitabu nao kwa hicho wakawa na hoja zilizo wazi? Lakini madhalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mnawaona hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu! Nionyesheni wameumba sehemu gani katika ardhi? Au wana ushirika wowote katika mbingu? Au tumewapa Kitabu nao kwa hicho wakawa na hoja zilizo wazi? Lakini madhaalimu hawaahidiani wao kwa wao ila udanganyifu tu. [40]

[40] Ewe Nabii! Waambie washirikina: Hebu nambieni, mmeiona hali ya hawa miungu wenu wa kishirikina mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Hebu nambieni, sehemu gani katika ardhi waliyo iumba wao? Hebu wanao ushirika wowote na Mwenyezi Mungu katika kuziumba mbingu? Sisi hatukuwapa kitabu cha ushirikina wakawa wao wanatoa hoja kutoka humo. Lakini wenye kudhulumu hawaahidiani wenyewe kwa wenyewe kwa uombezi wa miungu yao ya kumshirikisha na Mwenyezi Mungu ila kwa uwongo na kupambia pambia kuso mdanganya mtu ila aliye kuwa akili yake ni dhaifu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Nipasheni habari: Ni kitu gani cha ardhi ambacho washirika wenu wamekiumba? Au hawa washirika wenu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu wana ushirika na Allah Mtukufu katika uumbaji mbingu? Au tumewapa kitabu, hivyo basi wana ushahidi kutoka humo?» Lakini wakanushaji hawapeani ahadi isipokuwa udanganyifu na hadaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net