Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 39

Faatir 35:39

فاطر

هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَكُمْ خَلَـٰٓئِفَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ فَمَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُۥ ۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلْكَـٰفِرِينَ كُفْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ إِلَّا مَقْتًا ۖ وَلَا يَزِيدُ ٱلْكَـٰفِرِينَ كُفْرُهُمْ إِلَّا خَسَارًا

Maana

Yeye ndiye aliyekufanyeni wafuatizi (makhalifa) katika ardhi. Na anayekufuru, basi kufuru yake ni juu yake. Na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila hasara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye kufanyeni manaibu katika ardhi. Na anaye kufuru, basi kufuru yake ni juu yake; na kufuru za makafiri haziwazidishii kwa Mola wao Mlezi ila kuchukiwa. Wala kufuru za makafiri haziwazidishii ila khasara. [39]

[39] Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyeni baadhi yenu wawafuatie wengine katika kuiamirisha dunia na kuifanya itoe matunda yake. Na Yeye ni Mwenye kustahiki kushukuriwa si kukufuriwa. Basi mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu dhambi za kufuru yake zitakuwa juu yake mwenyewe. Na makafiri hawatopata ziada yoyote kwa Mola wao Mlezi isipo kuwa chuki na kukasirika. Wala makafiri hawatazidi ila kupata khasara tu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Ndiye Aliyewafanya nyinyi, enyi watu, baadhi yenu washikilie nafasi ya wengine katika ardhi. Basi Mwenye kukanusha upweke wa Allah Mtukufu miongoni mwenu madhara yake yatamrudia mwenyewe na ule ukafiri wake. Na hauwaongezei wakanushaji ule ukanushaji wao mbele ya Mola wao isipokuwa hasira na ghadhabu, na hakuwaongezei kule kumkanusha kwao Allah Mtukufu isipokuwa upotevu na maangamivu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net