Faatir 35:38
فاطرإِنَّ ٱللَّهَ عَـٰلِمُ غَيْبِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa siri za mbinguni na ardhi. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliomo vifuani. [38]
[38] Hakika Mwenyezi Mungu anajua vyema kila kilicho fichikana katika mbingu na ardhi. Hapana chenye kufichikana kwake. Na lau ange kukubalieni akakurudisheni duniani mngeli rejea yale yale aliyo kukatazeni. Hakika Yeye Mtukufu anavijua vyema vishawishi na vivutio viliomo ndani ya vifua.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika Allah Mtukufu Anakiona kila kisichoonekana mbinguni na ardhini, na kwa hakika Yeye ni Mjuzi mno wa vilivyojificha nyoyoni. Basi muogopeni Asiwaone mkiwa mko katika hali ya kudhamiria shaka au ushirikina katika kumpwekeshaYeye au juu ya unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani ziwashukie), au kuenda kinyume na amri Yake katika mambo madogo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net