Faatir 35:37
فاطروَهُمْ يَصْطَرِخُونَ فِيهَا رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ صَـٰلِحًا غَيْرَ ٱلَّذِى كُنَّا نَعْمَلُ ۚ أَوَلَمْ نُعَمِّرْكُم مَّا يَتَذَكَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَآءَكُمُ ٱلنَّذِيرُ ۖ فَذُوقُوا۟ فَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ
Na humo watapiga makelele: 'Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema siyo yale tuliyokuwa tukiyafanya.' Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakukujieni Mwonyaji? Basi onjeni! Kwani wale waliodhulumu hawana wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya. Kwani hatukukupeni umri wa kutosha kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Mwonyaji? Basi onjeni! Kwani walio dhulumu hawana wa kuwanusuru. [37]
[37] Na humo watapiga makelele kuomba msaada wakisema: Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni, tupate kutenda mema siyo yale tuliyo kuwa tukiyatenda duniani. Atawaambia: Hatukukupeni fursa ya kufanya a'mali, tukaufanya mrefu umri wenu kwa muda unao mkinika mtu ndani yake kuzingatia kwa mwenye kuzingatia? Na akukujieni Mtume akakuhadharisheni na adhabu hii. Basi onjeni katika Jahannamu malipo ya udhalimu wenu. Kwani mwenye kudhulumu hapati wa kumnusuru wala kumsaidia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa makafiri watapiga kelele kwa ukali wa adhabu ndani ya Moto wa Jahanamu wakiomba kuokolewa, «Mola wetu! Tutoe kwenye Moto wa Jahanamu na uturudishe duniani tupate kufanya matendo mema ambayo siyo yale tuliokuwa tukiyafanya katika uhai wetu wa duniani, tupate kuamini badala ya kukanusha.» Hapo Allah Mtukufu atawaambia, Kwani hatukuwapa katika kipindi cha uhai kadiri inayotosha ya umri kwa mwenye kutaka kuwaidhika awaidhike, na akawajia Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na pamoja na hivyo hamkuwaidhika? Basi onjeni adhabu ya Jahanamu! Kwani wenye kukanusha hawana msaidizi wa kuwaokoa na adhabu ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net