Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 36

Faatir 35:36

فاطر

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَهُمْ نَارُ جَهَنَّمَ لَا يُقْضَىٰ عَلَيْهِمْ فَيَمُوتُوا۟ وَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُم مِّنْ عَذَابِهَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى كُلَّ كَفُورٍ

Maana

Na wale waliokufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu. Hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyomlipa kila mwenye kuzidi ukafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahannamu, hawahukumiwi wakafa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri. [36]

[36] Na walio kufuru malipo yao waliyo ahidiwa ni Moto wa Jahannamu watakao uingia. Mwenyezi Mungu hatawahukumia mauti wakafa, wala hawatapunguziwa chembe ya adhabu wakapumzika. Ni kama hivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuendelea katika ukafiri na akaushikilia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliomkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake, watakuwa na Moto wa Jahanamu uliowashwa. Hakutatolewa uamuzi juu yao kuwa wafe wakapata kufa na kupumzika, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Mfano wa malipo hayo, Allah Mtukufu Anamlipa kila mwenye kuendelea kwenye ukafiri na kuwa na ukakamavu juu yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net