Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 45

Faatir 35:45

فاطر

وَلَوْ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُوا۟ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَآبَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرًۢا

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa yale waliyoyachuma, basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawaachilia mpaka ufike muda maalumu. Na muda wao ukifika, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake barabara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa waliyo yachuma, basi asingeli muacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja. Lakini Yeye anawachukulia mpaka ufike muda maalumu. Basi ukifika muda wao basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara. [45]

[45] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli kuwa anawaadhibu watu duniani, basi hapana shaka adhabu yake ingeli enea. Na asingeli muacha juu ya mgongo wa ardhi hata mnyama mmoja, kwa kuwa wote wametenda madhambi. Lakini anaakhirisha kuwaadhibu mpaka siku maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Basi ukifika muda wao walio wekewa atawalipa kwa uangalizi kaamili. Kwani Yeye ni Mwenye kuviona vitendo vya waja wake; hafichikiwi na kitu chochote katika hivyo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua kushinda wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Allah Mtukufu angewatesa watu kwa madhambi na maasia waliyoyatenda, asingeacha juu ya mgongo wa ardhi mnyama yoyote anayetembea juu yake. Lakini Anawapa mhula na Anachelewesha kuwaadhibu mpaka wakati maalumu Aliyoupanga. Na wakati wa kuwaadhibu ukija, basi Allah Mtukufu kwa waja Wake ni Mjuzi, hakuna yoyote kati yao atakayefichika Kwake, na hakuna chochote miongoni mwa mambo yao kilicho mbali na ujuzi Wake, na Atawalipa wao kwa walichotenda, chema au kibaya.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net