Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Faatir
Sura ya 35

Faatir

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 45

وَلَوْ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِمَا كَسَبُوا۟ مَا تَرَكَ عَلَىٰ ظَهْرِهَا مِن دَآبَّةٍ وَلَـٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِعِبَادِهِۦ بَصِيرًۢا 45

{45} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akataja ukamilifu wa ustahamilivu wake, na wingi wa kuwapa kwake muhula vigogo wa kufanya uhalifu na madhambi, akasema: "Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwachukulia watu kwa yale waliyoyachuma" miongoni mwa dhambi, "basi asingelimuacha juu ya ardhi hata mnyama mmoja." Yaani, adhabu hiyo ingewajumuisha hata wanyama ambao hawajajukumishwa kisheria. "Lakini" Mwenyezi Mungu huwapa muhula na wala haghafiliki mbali nao "mpaka ufike muda maalumu. Na muda wao ukifika, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake baraabara." Na hapo atawalipa kulingana na aliyoyajua kuwahusu,ya heri na maovu.

Imekamilika tafsiri ya Surat Fatir Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.