Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 3

Faatir 35:3

فاطر

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَـٰلِقٍ غَيْرُ ٱللَّهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۚ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ

Maana

Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu. Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnako geuzwa? [3]

[3] Enyi watu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu, kwa kuzishukuru na kutimiza haki yake. Na mkiri hayo yaliyo tokea ndani ya nafsi zenu, ya kwamba hapana muumba isipo kuwa Mwenyezi Mungu ambaye anakuruzukuni kutoka mbinguni kwa zinavyo viteremsha, na kutoka kwenye ardhi kwa vinavyo toka humo, ambavyo vinakuleteeni uhai wenu. Hapana mungu isipo kuwa Yeye anaye waruzuku waja wake. Basi yawaje mnavyo geuzwa mkaacha Tawhidi ya Muumba wenu na Mwenye kukuruzukuni mkaendea kumshirikisha katika ibada yake?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Kumbukeni, kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu, neema ya Allah Mtukufu juu yenu. Hakuna muumba wenu isipokuwa Allah Mtukufu, Anayewaruzuku nyinyi kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa maji, madini na vinginevyo kutoka ardhini. Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiye na mshirika. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na kumpwekesha?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net