Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Faatir
Sura ya 35

Faatir

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 3

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱذْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَـٰلِقٍ غَيْرُ ٱللَّهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۚ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ 3

{3} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha watu wote kukumbuka neema zake juu yao, na hili linajumuisha kuzitaja kwa moyo kwa kuzikiri, na kwa ulimi kwa kusifu, na kwa viungo kwa kutii. Kwani kutaja neema zake Mtukufu ni sababu ya kumshukuru. Kisha akawatanabahisha juu ya neema za kimsingi ambazo ni kuwaumba na kuwaruzuku, na akasema: "Ati yupo muumba mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayekupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi?" Na kwa kuwa inajulikana vyema kuwa hakuna yeyote anayeumba na anayeruzuku isipokuwa Mwenyezi Mungu; ikatokea kutokana na hili kuwa huu ni ushahidi wa uungu wake na umola wake, na ndiyo maana akasema: "Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Basi wapi mnakogeuzwa?" Yaani, kwa nini mnageuzwa mkaacha kumwabudu Muumba, Mwenye kuruzuku na mkaanza kumuabudu kiumbe anayeruzukiwa.