Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 4

Faatir 35:4

فاطر

وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ ۚ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ

Maana

Na wakikukanusha, basi walikwisha kanushwa Mitume kabla yako. Na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakikukanusha, basi walikwisha kanushwa Mitume kabla yako. Na mambo yote yatarudishwa kwa Mwenyezi Mungu. [4]

[4] Na hao makafiri wa kaumu yako wakikukadhabisha kwa uwongofu ulio waletea, basi wewe wastahamilie. Kwani Mitume wa kabla yako walikwisha kadhibishwa vile vile, na wakavumilia kwa walivyo kadhibishwa mpaka wakashinda. Na mambo yote yatarejea kwa Mwenyezi Mungu peke yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na watu wako wakikukanusha, ewe Mtume, kwa hakika wamekanushwa Mitume kabla yako wewe. Na kwa Allah Mtukufu mambo yanaishia huko Akhera, basi hapo Atamlipa kila mmoja anachostahili. Katika aya hii pana kumliwaza Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net