Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 35 · Aya ya 5

Faatir 35:5

فاطر

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا ۖ وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ

Maana

Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi kamwe yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala kamwe yule mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Basi yasikudanganyeni maisha ya dunia, wala mdanganyifu asikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu. [5]

[5] Enyi watu! Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu, juu ya mambo ya kufufuliwa, na malipo, na ushindi, ni haki ya kweli. Basi msiache dunia ikakukhadaini na Akhera. Wala Shetani akakukhadaini mkaacha kuwafuata Mitume, na akakupeni tamaa kuwa mtasamehewa na hali huku mnaendelea na maasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi watu! Hakika agizo la Allah Mtukufu la Ufufuzi, malipo mema na mateso ni kweli iliyothibiti, basi yasiwadanganye maisha ya duniani kwa matamanio yake na matakwa yake, wala asiwadanganye Shetani kuhusu Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Faatir

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net