Faatir 35:2
فاطرمَّا يَفْتَحِ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ مِن رَّحْمَةٍ فَلَا مُمْسِكَ لَهَا ۖ وَمَا يُمْسِكْ فَلَا مُرْسِلَ لَهُۥ مِنۢ بَعْدِهِۦ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ
Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu, hapana wa kuizuia. Na anayoizuia, hapana wa kuiachilia isipokuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Rehema ambayo Mwenyezi Mungu anawafungulia watu hapana wa kuizuia. Na anayo izuia hapana wa kuipeleka isipo kuwa Yeye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [2]
[2] Mwenyezi Mungu akipeleka rehema kwa watu, rehema yoyote ile iwayo, ikiwa ni mvua, au neema, au amani, au hikima - hapana mtu yeyote awezaye kuwazuilia na kuwanyima. Na chochote katika hivyo akikizuilia Yeye basi hapana mmoja awezaye kukifungulia isipo kuwa Yeye Mwenyewe. Na Yeye ndiye Mwenye kushinda ambaye hashindwi. Mwenye hikima asiye kosea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Chochote kile Anachowafungulia watu Allah Mtukufu miongoni mwa riziki, mvua, afya, ujuzi na neema nyinginezo, hakuna yoyote wa kuzuia rehema hii, na chochote kile anachokizuia hakuna yoyote baada Yake, Kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, anayeweza kukiachilia. Na Yeye Ndie Mshindi Mwenye kukitendesha nguvu kila kitu, Mwingi wa hekima Ambaye Anaiachilia rehema na Anaizuia kulingana na hekima Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net