Saba 34:28
سبإوَمَآ أَرْسَلْنَـٰكَ إِلَّا كَآفَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui. [28]
[28] Na Sisi hatukukutuma ewe Muhammad, ila kwa watu wote. Uwe ni mwenye kuwabashiria Waumini kuwa watapata kheri, na mwenye kuwaonya makafiri kuwa watapata shari. Lakini aghlabu ya watu hawaujui ukweli wako, wala kuwa Utume wako ni wa kwa watu wote. (Haya ni kwa sababu hapana Mtume aliye kuja kwa watu wote ila huyu Nabii Muhammad s.a.w. Nabii Musa alikuja kwa Wana wa Israili kuwatoa Misri. Nabii Isa, Yesu Kristo, pia kaja kwa Wana wa Israili tu, kama isemavyo Qur'ani 3.49, na Injili ya Mathayo 10.5-6 Yesu alipo sema: "Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Na 15.24 alipo sema: "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." Na Injili ya Yohana 17.9)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hatukukutuma, ewe Mtume, isipokuwa ni kwa watu wote, uwabashirie malipo mema ya Allah Mtukufu na uwaonye na adhabu Yake. Lakini wengi wa watu hawaijui haki, hivyo basi wao wanaipa mgongo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net