Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 27

Saba 34:27

سبإ

قُلْ أَرُونِىَ ٱلَّذِينَ أَلْحَقْتُم بِهِۦ شُرَكَآءَ ۖ كَلَّا ۚ بَلْ هُوَ ٱللَّهُ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Maana

Sema: Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Nionyesheni mlio waunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [27]

[27] Waambie: Nionyesheni hao mlio waunganisha na Mwenyezi Mungu kwa kustahiki kuabudiwa, mnao dai kuwa ni miungu wa shirika na Yeye. Yeye hana mshirika, bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima katika kupanga kwake na kuendesha kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, Nionesheni kwa hoja na dalili wale mliyowaunganisha na Allah Mtukufu mkawafanya ni washirika Wake katika kuabudiwa, je wao wameumba chochote? Mambo si kama walivyoeleza.Bali Yeye Ndiye Mwenye kuabudiwa kwa haki, ambaye hana mshirika, aliye Mshindi katika kuwatesa waliomshirikisha, na mwenye hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake na upelekeshaji mambo ya viumbe Vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net