Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 26

Saba 34:26

سبإ

قُلْ يَجْمَعُ بَيْنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفْتَحُ بَيْنَنَا بِٱلْحَقِّ وَهُوَ ٱلْفَتَّاحُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu, Mwenye kujua vyema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu Mwenye kujua. [26]

[26] Waambie: Mola wetu Mlezi atatukusanya Siku ya Kiyama, kisha atatuhukumu kwa haki. Na Yeye Subhanahu ndiye Hakimu wa kila shauri, Mwenye kujua kwa hakika yetu sisi na yenu nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, «Mola wetu Atatukusanya baina yetu na nyinyi Siku ya Kiyama, kisha Atatoa uamuzi wa uadilifu baina yetu. Na Yeye Ndiye Mfunguzi Mwenye kutoa uamuzi baina ya viumbe Vyake, Mwingi wa ujuzi wa yale yanayotakikana yatolewe uamuzi na hali ya viumbe Vyake. Hakuna kinachofichika Kwake chochote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net