Saba 34:29
سبإوَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Na wanasema: "Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanasema: Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli? [29]
[29] Na makafiri wanasema kwa kuifanya haiwi hiyo Siku iliyo ahidiwa kwa ajili ya malipo: Lini itakuwa ahadi hii tuingie Motoni, na nyinyi muingie Peponi, kama nyinyi ni wakweli kwa hiyo ahadi yenu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa washirikina wanasema kwa njia ya shere, «Ni lini wakati wa Ahadi hii ambayo unatuahidi kuwa Allah Mtukufu Atatukusanya ndani yake kisha Ahukumu baina yetu, iwapo nyinyi ni wakweli katika kile mlichotuahidi kwacho?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net