Saba 34:30
سبإقُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوْمٍ لَّا تَسْتَـْٔخِرُونَ عَنْهُ سَاعَةً وَلَا تَسْتَقْدِمُونَ
Sema: "Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtakawiya mbali nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia. [30]
[30] Ewe Nabii! Waambie: Miadi yenu ni Siku kubwa mno; ikifika hamto chelewa hata kwa saa moja, wala hamto tangulia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, «Nyinyi mna maagano ambayo hapana budi yatawajia, nayo ni maagano ya Siku ya Kiyama, hamtachelewa nayo hata muda mchache wa kupata kutubia, na wala hamtatangulia mbele yake mkaadhibiwa hata kwa muda mchache. Basi jihadharini na Siku hiyo na jitayarisheni kwa vifaa vyake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net