Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 31

Saba 34:31

سبإ

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ بِهَـٰذَا ٱلْقُرْءَانِ وَلَا بِٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ ۗ وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّـٰلِمُونَ مَوْقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمْ يَرْجِعُ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ ٱلْقَوْلَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ لَوْلَآ أَنتُمْ لَكُنَّا مُؤْمِنِينَ

Maana

Na walisema wale waliokufuru, "Hatutaiamini Qur-ani hii, wala yale yaliyokuwa kabla yake." Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia wale waliotakabari, "Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema walio kufuru: Hatutaiamini Qur'ani hii, wala yaliyo kuwa kabla yake. Na ungeli waona madhaalimu watapo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia walio takabari: Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungeli kuwa Waumini sisi. [31]

[31] Na walio kufuru wanasema: Hatuisadiki Qur'ani hii wala hivyo Vitabu vilivyo tangulia kabla yake kwa hayo vinavyo amrisha na kulingania. Na lau ungeli ona - ewe mwenye kuweza kuona - wakati wanapo simamishwa madhaalimu mbele ya Muumba wao, Mwenye kumiliki amri yao, ungeliona maajabu katika msimamo wao, pale wanapo jibizana maneno wao kwa wao. Walio wanyonge wakiwaambia walio tukuka juu yao: Ingeli kuwa si nyinyi, kwa kutusaliti na kutamalaki, hapana shaka tungeli kuwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na waliokanusha walisema, «Hatutaiamini hii Qur’ani wala vile vilivyoitangulia, kina Taurati, Injili na Zaburi.» Kwa hakika washakanusha vitabu vyote vya Allah Mtukufu. Na lau utaona pindi madhalimu watafungwa mbele ya Mola wao ili wahesabiwe, huku wakirudishiana maneno baina yao, kila mmoja anamtupia lawama mwingine, utaona jambo la kutisha! Watakuwa waliokuwa wakifanywa wanyonge wakisema kuwaambia wale waliokuwa na kiburi, nao ni wale viongozi na wakubwa waliopotea na kupoteza, «Lau si nyinyi kutupoteza njia tungekua ni wenye kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net