Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 32

Saba 34:32

سبإ

قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتُضْعِفُوٓا۟ أَنَحْنُ صَدَدْنَـٰكُمْ عَنِ ٱلْهُدَىٰ بَعْدَ إِذْ جَآءَكُم ۖ بَلْ كُنتُم مُّجْرِمِينَ

Maana

Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge, "Kwani sisi ndio tuliwazuia na uongofu baada ya huo kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wahalifu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walio takabari watawaambia wanyonge: Kwani sisi ndio tulio kuzuieni na uwongofu baada ya kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wakosefu. [32]

[32] Walio takabari na wakajiona ni wakubwa, watawaambia wanyonge, kwa kuyapinga maneno yao: Kwani sisi tulikuzuieni msiongoke ulipo kufikieni uwongofu? Tumekuzuieni sisi au nyinyi wenyewe ndio mmekhiari upotofu kuliko uwongofu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Viongozi watasema kuwaambia wale waliofanywa wanyonge, «Kwani ni sisi tuliowazuia uongofu baada ya kuwajia? Bali ni nyinyi wenyewe mlikuwa wahalifu kwa kuwa mliingia kwenye ukafiri kwa matakwa yenu na hiyari yenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net