Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 10

Saba 34:10

سبإ

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا دَاوُۥدَ مِنَّا فَضْلًا ۖ يَـٰجِبَالُ أَوِّبِى مَعَهُۥ وَٱلطَّيْرَ ۖ وَأَلَنَّا لَهُ ٱلْحَدِيدَ

Maana

Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, tukasema: "Enyi milima, karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia." Na tukamlainishia chuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, (tukasema): Enyi milima! Karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia. Na tukamlainishia chuma. [10]

[10] Wallahi! Kwa hakika tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu kwa kumpa hikima na Kitabu. Na tulisema: Enyi milima! Karirini pamoja naye Tasbihi kumtakasa Mwenyezi Mungu, pale anapo sabihi yeye. Na Sisi tuliwafanya ndege pia wamtumikie, nao wawe wakikariri kumtakasa Mwenyezi Mungu. Na tukakifanya chuma kiwe laini kwake aunde kwa sura atakayo. Daudi, a.s. ni mmoja wa Manabii wa Wana wa Israili, na mmoja wa wafalme wao. Aliishi katika zama za baina ya mwaka 1010 na 970 K.K. (yaani kabla ya kuzaliwa Nabii Isa a.s.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tulimpa Dāwūd unabii, Kitabu na ujuzi, na tukayaambia majabali na ndege, «Takaseni pamoja naye!» (Dāwūd anapomtakasa Allah Mtukufu kwa kuleta tasbihi, fanyeni hivyo pamoja naye). Na tulimlainishia chuma kikawa ni kama unga uliokandwa, Anakifinyanga anavyotaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net