Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 9

Saba 34:9

سبإ

أَفَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَىٰ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ ۚ إِن نَّشَأْ نَخْسِفْ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ نُسْقِطْ عَلَيْهِمْ كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ

Maana

Kwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao ya mbingu na ardhi? Tungeli penda tungeli wadidimiza ndani ya ardhi, au tungeli wateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliye tubia. [9]

[9] Je! Wamepofuka, hata hawaaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao ya mbinguni na katika ardhi wakaujua uweza wetu wa kutenda tuyatakayo? Tukitaka ardhi iwameze, tutawazamisha. Au tungeli taka viwaangukie vipande vya mbingu tuwasage sage tungeli wateremshia. Hakika katika tuliyo yataja zipo dalili kwa kila mja mwenye kurejea kwa Mola wake Mlezi katika kila jambo lake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawaoni makafiri hawa wasioamini Akhera ukubwa wa uwezo wa Allah Mtukufu juu ya vilivyoko mbele yao na nyuma yao, miongoni mwa mbingu na ardhi, vinavyoshangaza akili, na kwamba viwili hivyo vimewazunguka? Tutakapo tutawazamisha ndani ya ardhi, kama tulivyomfanyia Qārūn, au tutawateremshia vipande vya adhabu, kama tulivyowafanyia watu wa Shu‛ayb, kwa hakika mbingu iliwanyeshea moto ukawaunguza. Hakika katika hilo tulilolitaja la uwezo wetu kuna ushahidi wazi kwa kila mja mwenye kurudi kwa Mola wao kwa kutubia, mwenye kukubali upweke Wake na mwenye kumtakasia ibada.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net