Saba 34:8
سبإأَفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَم بِهِۦ جِنَّةٌۢ ۗ بَلِ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ فِى ٱلْعَذَابِ وَٱلضَّلَـٰلِ ٱلْبَعِيدِ
Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au ana wazimu. Bali wale wasioamini Akhera wamo adhabuni na upotovu wa mbali kabisa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au ana wazimu. Bali wasio amini Akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa. [8]
[8] Mtu huyu amemzulia uwongo Mwenyezi Mungu kwa kumnasibishia kuwa atawafufua wafu, au mtu huyu ana wazimu ndio anasema asiyo yajua? Siyo hayo wayasemayo. Bali ukweli wa mambo ni kuwa hao wasio iamini Akhera wataingia katika adhabu na upotovu wa kupotelea mbali na Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani mtu huyu amemzulia Allah Mtukufu urongo, au ana wazimu na kwa hivyo anasema jambo asilolijua? Mambo si vile kama wanavyosema makafiri, bali Muhammad ni mkweli wa wakweli. Na wale wasioamini kufufuliwa na wasiofanya matendo ya kuwafaa huko, watakuwa kwenye adhabu ya milele huko Akhera, na wako kwenye upotevu wa mbali hapa duniani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net