Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 7

Saba 34:7

سبإ

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هَلْ نَدُلُّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ يُنَبِّئُكُمْ إِذَا مُزِّقْتُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمْ لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍ

Maana

Na wale waliokufuru walisema: Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio kufuru walisema: Je! Tukujuulisheni mtu anaye kuambieni kwamba mtakapo chambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya? [7]

[7] Na makafiri waliambiana wenyewe kwa wenyewe, kwa kufanyia kejeli kufufuliwa: Je! Tukuonyesheni mtu ataye kuambieni kwamba mtapo kwisha kufa, na viwiliwili vyenu vikagawika mapande mapande kuwa ati mtafufuliwa tena kwa umbo jipya?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri walisema, wakiambiana wao kwa wao kwa njia ya shere, «Je, tuwaoneshe mtu (wakimkusudia Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) atakayewaambia kwamba nyinyi mkifa na miili yenu ikawa mbalimbali kabisa kuwa nyinyi mtahuishwa na mtafufuliwa kutoka makaburini mwenu?» wamesema hayo kwa kupita kiasi katika kukanusha kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net