Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 11

Saba 34:11

سبإ

أَنِ ٱعْمَلْ سَـٰبِغَـٰتٍ وَقَدِّرْ فِى ٱلسَّرْدِ ۖ وَٱعْمَلُوا۟ صَـٰلِحًا ۖ إِنِّى بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Tukamwambia: "Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Tukamwambia:) Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayo yatenda. [11]

[11] Tulimfunulia kumwambia aunde nguo za chuma pana za kujilinda katika vita na maadui. Naye azifume kwa hikima na ustadi katika kuviunga viungo vyake. Na tukamwambia yeye na watu wake: Tendeni yatakayo kuleteeni kheri na maslaha. Hakika Mimi nayaona vyema yote myatendayo, hapana kinacho niporonyoka nisikione.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

(Na tulikwambia, ewe Dāwūd,) «Tengeneza nguo za chuma zilizotimia na zilizo pana, na ukadirie vipimo vya misumari katika vidani vya kuunganisha nguo hizo za chuma, na usikifanye kidani kuwa kidogo kwani kitakuwa dhaifu, na kwa hivyo hizo nguo za chuma hazitaweza kumkinga (mwenye kuzivaa). Na usizifanye kubwa zikawa nzito kwa mwenye kuzivaa. Na ufanye, ewe Dāwūd, wewe na watu wako, vitendo vya kumtii Allah Mtukufu, kwani mimi kwa mnayoyafanya ni Mwenye kuyaona, hakifichiki kwangu kitu chochote katika hivyo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net