Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 12

Saba 34:12

سبإ

وَلِسُلَيْمَـٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهْرٌ وَرَوَاحُهَا شَهْرٌ ۖ وَأَسَلْنَا لَهُۥ عَيْنَ ٱلْقِطْرِ ۖ وَمِنَ ٱلْجِنِّ مَن يَعْمَلُ بَيْنَ يَدَيْهِ بِإِذْنِ رَبِّهِۦ ۖ وَمَن يَزِغْ مِنْهُمْ عَنْ أَمْرِنَا نُذِقْهُ مِنْ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Maana

Naye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majini walikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anaye jitenga na amri yetu katika wao, tunamwonjesha adhabu ya Moto unao waka. [12]

[12] Na Suleiman tukamfanyia upepo umtumikie. Mwendo wake wakati wa asubuhi mmoja ni sawa na safari ya dasturi inayo chukua mwezi mzima. Na mwendo wake wakati wa jioni moja ni kama safari ya kuchukua mwezi. Na tukamyayushia maadeni ya shaba ikawa inatiririka kwa wingi moja kwa moja. Na tukawafanya majini wawe wakimtumikia mbele yake kwa amri ya Mola wake Mlezi. Na yeyote katika majini aliye wacha kut'ii amri ya Suleiman basi tulimwonjesha adhabu ya Moto unao waka kwa nguvu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tulimdhalilishia Sulaymān upepo, ukawa unatembea kutoka mwanzo wa mchana mpaka katikati yake mwendo wa mwezi, na kutoka katikati ya mchana mpaka usiku mwendo wa mwezi kwa mwendo wa kawaida. Na tulimyayushia shaba ikawa inatiririka kama vile maji yanavyotiririka, akawa anafanya kwa shaba hiyo anachotaka. Na tulimdhalilishia miongoni mwa majini wenye kutumika mbele yake, na yoyote kati yao anayesita kufuata amri yetu tuliomuamrisha ya kumtii Sulaymān tutamuonjesha kutokana na adhabu ya Moto unaowaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net