Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 13

Saba 34:13

سبإ

يَعْمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَـٰرِيبَ وَتَمَـٰثِيلَ وَجِفَانٍ كَٱلْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَـٰتٍ ۚ ٱعْمَلُوٓا۟ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِىَ ٱلشَّكُورُ

Maana

Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyo ondolewa mahala pake. Enyi watu wa Daudi! Fanyeni kazi kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru. [13]

[13] Hao majini wakifanya atakacho Suleiman, kama misikiti kwa ajili ya ibada, na masanamu, na madeste au mabakuli makubwa kama mahodhi ya maji, na vyombo vya kupikia, yaani masufuria, makubwa yaliyo kaa pale pale penye mafya yake hayaondoki kwa kuwa ni makubwa mno. Na tukawaambia watu wa Daudi: Tendeni kazi ya kumshukuru Mwenyezi Mungu vilivyo. Na ni wachache miongoni mwa waja wangu ambao wanakumbuka neema zangu wakawa wananishukuru kwa wingi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Majini wanamfanyia Sulaymān anachotaka miongoni mwa misikiti ya ibada, picha za shaba na ukoa, madishi makubwa kama mabirika ya kukusanyika maji ndani yake na vyungu vilivyojikita visivyotikisika kutoka mahali pake kwa ukubwa wake, na tukasema, «Enyi jamii ya Dăwūd! Fanyeni kwa kumshukuru Allah Mtukufu kwa kile Alichowapa, kwa kumtii na kufuata amri Yake.» Na ni wachache, miongoni mwa waja wangu, wenye kumshukuru Allah Mtukufu kwa wingi. Na Dāwūd, yeye na jamii yake, alikuwa miongoni mwa hao wachache.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net