Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 14

Saba 34:14

سبإ

فَلَمَّا قَضَيْنَا عَلَيْهِ ٱلْمَوْتَ مَا دَلَّهُمْ عَلَىٰ مَوْتِهِۦٓ إِلَّا دَآبَّةُ ٱلْأَرْضِ تَأْكُلُ مِنسَأَتَهُۥ ۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ ٱلْجِنُّ أَن لَّوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ ٱلْغَيْبَ مَا لَبِثُوا۟ فِى ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ

Maana

Na tulipomhukumia kufa, hapana aliyewajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Na alipoanguka, majini wakatambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulipo mhukumia kufa, hapana aliye wajuulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliye kula fimbo yake. Na alipo anguka majini walitambua lau kuwa wangeli jua ya ghaibu wasingeli kaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha. [14]

[14] Tulipo mhukumia Suleiman mauti, hapana aliye waonyesha majini kuwa kesha kufa ila kinyama cha ardhi kilicho ila fimbo yake aliyo kuwa akiiegemea. Alipo anguka majini wakajua kuwa lau kuwa wangeli jua ya ghaibu wasingeli endelea na ile adhabu ya mashaka ya kuwadhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tulipopitisha kuwa Sulaymān afe, hakuna kilichowafahamisha majini juu ya kifo chake isipokuwa mchwa kuila fimbo yake ambayo alikuwa ameiegemea, basi Sulaymām akaanguka chini, na hapo majini wakajua kwamba wao lau wangekua wanajua ghaibu wasingekaa kwenye adhabu yenye kudhalilisha na kazi ngumu kumfanyia Sulaymān, kwa wao kudhania kuwa yeye ni katika walio hai. Katika hii aya kuna kubatilisha itikadi ya baadhi ya watu kwamba majini wanayajua yasiyoonekana. Kwani lau wao wangeyajua yasiyoonekana wangejua kifo cha Sulaymān, amani imshukie, na wasingekaa kwenye adhabu yenye kunyongesha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net