Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 15

Saba 34:15

سبإ

لَقَدْ كَانَ لِسَبَإٍ فِى مَسْكَنِهِمْ ءَايَةٌ ۖ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٍ وَشِمَالٍ ۖ كُلُوا۟ مِن رِّزْقِ رَبِّكُمْ وَٱشْكُرُوا۟ لَهُۥ ۚ بَلْدَةٌ طَيِّبَةٌ وَرَبٌّ غَفُورٌ

Maana

Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika ilikuwapo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu. [15]

[15] Ninaapa: Hakika katika watu wa Sabaa katika makaazi yao ya Yaman palikuwa na Ishara ya uweza wetu. Zilikuwako bustani mbili zilizo zunguka nchi yao, kulia na kushoto. Wakaambiwa: Kuleni katika riziki ya Mola wenu Mlezi, na mshukuru neema zake kwa kuzitumilia inavyo faa. Huu mji wenu ni mji mzuri, una vivuli na matunda. Na Mola wenu Mlezi ni Mwingi wa maghfira kwa anaye mshukuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika, kabila la Saba’ la huko Yaman, kwenye makazi ya watu wake kuna dalili ya uwezo wetu: mabustani mawili kuliani na kushotoni, «Kuleni riziki ya Mola wenu na mumshukuruni kwa neema Zake juu yenu, kwani nchi yenu ina mchanga bora na hewa nzuri, na Mola wenu ni Mwingi wa msamaha kwenu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net