Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 16

Saba 34:16

سبإ

فَأَعْرَضُوا۟ فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ سَيْلَ ٱلْعَرِمِ وَبَدَّلْنَـٰهُم بِجَنَّتَيْهِمْ جَنَّتَيْنِ ذَوَاتَىْ أُكُلٍ خَمْطٍ وَأَثْلٍ وَشَىْءٍ مِّن سِدْرٍ قَلِيلٍ

Maana

Lakini wakayapa mgongo. Kwa hivyo, tukawatumia mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda makali, machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini wakaacha. Tukawapelekea mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyengine zenye matunda makali machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi. [16]

[16] Lakini wao waliacha kushukuru neema, na wakawa maisha yao ya kiburi. Tukawafungulia mafuriko ya nguvu yaliyo tokea baada ya kupasuka kuta za mahodhi, yakateketeza mabustani yao. Tukawabadilishia badala ya bustani zao mbili zile zenye matunda mazuri, zikawa nyengine mbili zenye matunda machungu, na miti isiyo kuwa na matunda, na mikunazi kidogo isiyo toa hamu. Hili liitwalo "Hodhi" la maji ya mvua kubwa au "Hodhi la Ma`arib" ni kubwa kuliko mahodhi yote ya Yaman. Hodhi hili linaweza kubadilisha ardhi kavu ya kiasi ya maili 300 ya mraba ikawa yenye rutba na mashamba. Na dalili ya hayo ni hizo bustani mbili zilizo tajwa. Wanazuoni wa taarikh (historia) wanakhitalifiana katika ujenzi wa hilo hodhi kuu. Vile vile zipo kauli mbali mbali kukhusu kubomoka kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakaipa mgongo amri ya Allah Mtukufu, wakaacha kumshukuru na wakawakanusha Mitume, tukawatumia mafuriko yenye kubomoa yaliyo na nguvu, yaliyoliharibu bwawa la maji na yakayazamisha mabustani. Na tukawageuzia mabustani yao mawili yenye kutoa matunda yakawa ni mabustani mawili yenye miti michache ya khamṭ, nayo ni miti ya matunda machungu yenye ladha ya kuchukiza, na athl, nayo ni miti inayofanana na ṭarfā’ isiyokuwa na matunda, na mikunazi michache yenye miba mingi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net