Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 17

Saba 34:17

سبإ

ذَٰلِكَ جَزَيْنَـٰهُم بِمَا كَفَرُوا۟ ۖ وَهَلْ نُجَـٰزِىٓ إِلَّا ٱلْكَفُورَ

Maana

Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyo kufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipo kuwa anaye kufuru? [17]

[17] Hayo ndiyo malipo tuliyo walipa kwa kufuru zao kuzikufuru neema na kuto zishukuru. Na kwani Sisi tunamuadhibu kwa adhabu hii kali yeyote yule ila aliye kuwa mwingi wa kumkufuru Mwenyezi Mungu na fadhila zake?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mabadiliko hayo, kutoka kwenye mambo mazuri kwenda kwenye mabaya, ni kwa sababu ya kukanusha kwao na kutoshukuru kwao neema za Allah Mtukufu. Na hatumtesi mateso haya makali isipokuwa mkanushaji sana aliyeendelea kwenye ukanushaji; atalipwa kulingana na matendo yake, sawa kwa sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net