Saba 34:18
سبإوَجَعَلْنَا بَيْنَهُمْ وَبَيْنَ ٱلْقُرَى ٱلَّتِى بَـٰرَكْنَا فِيهَا قُرًى ظَـٰهِرَةً وَقَدَّرْنَا فِيهَا ٱلسَّيْرَ ۖ سِيرُوا۟ فِيهَا لَيَالِىَ وَأَيَّامًا ءَامِنِينَ
Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia, "Nendeni humo usiku na mchana kwa amani."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na baina yao na miji mingine tuliyo ibariki tuliweka miji iliyo dhaahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana kwa amani. [18]
[18] Na tulifanya baina ya maskani yao ya Yaman na baina ya miji mingine iliyo barikiwa miji mingineyo pia iliyo karibiana inaonana. Na tukafanya makhusiano baina yao ni kiasi maalumu cha mwendo usio kuwa wa taabu. Na tukawaambia: Nendeni humo usiku na mchana nanyi mko katika amani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulijaalia, baina ya watu wa Saba’, na hali wao wako Yaman, na ile miji tuliobarikia, nayo ni Shām, kuwe na miji iliyoshikana, aliye kwenye mji wowote kati ya hiyo huuona mji mwingine. Na tukafanya mwendo wa kutembea humo ni mwendo uliokadiriwa, kutoka nyumba hadi nyumba, bila mashaka, na tukawaambia, «Nendeni kwenye miji hiyo, wakati muutakao wa usiku au mchana, mkiwa mko kwenye amani hamuogopi adui, njaa wala kiu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net