Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 19

Saba 34:19

سبإ

فَقَالُوا۟ رَبَّنَا بَـٰعِدْ بَيْنَ أَسْفَارِنَا وَظَلَمُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَجَعَلْنَـٰهُمْ أَحَادِيثَ وَمَزَّقْنَـٰهُمْ كُلَّ مُمَزَّقٍ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ

Maana

Lakini wakasema, "Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu." Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini wakasema: Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu. Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru. [19]

[19] Kwa kutakabari kwa neema, na raha, na amani, walisema: Tuwekee mbali masafa ya safari zetu, tusisadifu kukuta miji iliyo amirishwa ya katikati mpaka tufike huko twendako! Mwenyezi Mungu akazifanya ziwe mbali hizo safari zao. Na wakawa wao wamejidhulumu nafsi zao kwa uasi wao. Tukawafanya hao ni masimulizi ya watu, na tukawatenganisha mtengano mkubwa. Hakika katika yaliyo wapata hao yapo mawaidha kwa kila mwenye kusubiri kwa balaa, mwenye kushukuru kwa apewacho.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa sababu ya kuruka mipaka kwao, walichoka na raha na amani na maisha ya neema na wakasema, «Mola wetu! Ifanye miji yetu iwe mbali mbali ili safari zetu zirefuke baina ya miji hiyo, tusipate mji ulioimarika njiani tunapokwenda.» Na wakajidhulumu nafsi zao kwa kukanusha kwao, na kwa hivyo tukawaangamiza na tukawafanya ni mazingatio na mazungumzo kwa wanaokuja baada yao, na tukawatenganisha kila namna ya kuwatenganisha, na miji yao ikawa magofu. Kwa hakika yale yaliyoikumba Saba’ ni mazingatio kwa kila mwingi wa uvumilivu juu ya shida na mambo magumu, mwingi wa kushukuru neema za Allah Mtukufu Aliyetukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net