Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 20

Saba 34:20

سبإ

وَلَقَدْ صَدَّقَ عَلَيْهِمْ إِبْلِيسُ ظَنَّهُۥ فَٱتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقًا مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na bila ya shaka Iblisi alihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipo kuwa kundi la Waumini. [20]

[20] Na bila ya shaka Iblisi amehakikisha dhana yake juu yao. Nao wakamfuata yeye isipo kuwa wachache miongoni mwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa hakika alidhani Iblisi dhana isiyo ya ukweli kuwa atawapoteza wanadamu na kwamba wao watamtii yeye katika kumuasi Allah Mtukufu, na dhana yake kwao ikawa ya kweli, kwa kuwa wao walimtii yeye na wakamuasi Mola wao, isipokuwa kundi la wenye kumuamini Allah Mtukufu, kwani wao walijikita kwenye utiifu wa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net