Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 21

Saba 34:21

سبإ

وَمَا كَانَ لَهُۥ عَلَيْهِم مِّن سُلْطَـٰنٍ إِلَّا لِنَعْلَمَ مَن يُؤْمِنُ بِٱلْـَٔاخِرَةِ مِمَّنْ هُوَ مِنْهَا فِى شَكٍّ ۗ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ حَفِيظٌ

Maana

Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, isipokuwa kwa sababu ya kuwajaribu ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, ila kwa sababu ya kuwajaribu tujue nani mwenye kuamini Akhera, na nani anaye tilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu. [21]

[21] Na wala Iblisi hakuwa na nguvu za kuwafanya wamt'ii na kumnyenyekea; lakini Mwenyezi Mungu kawafanyia mtihani apate kuwadhihirisha wepi wanao isadiki Akhera, na wepi wana shaka nayo. Ewe Nabii! Mola wako Mlezi ni Mwenye kuchungua kila kitu, Mwenye kusimamia kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wala hakuwa iblisi na uwezo wa kuwalazimisha wakanushaji kukufuru, lakini hekima ya Allah Mtukufu imepitisha awapambie wanadamu ili ujitokeze ujuzi Wake wa kale, tupate kumpambanua anayeamini kufufuliwa, thawabu na adhabu na kumtenganisha na yule mwenye shaka na hilo. Na Mola wako ni Mtunzi wa kila jambo, Analihifadhi na kutoa malipo yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net