Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 34 · Aya ya 22

Saba 34:22

سبإ

قُلِ ٱدْعُوا۟ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُۥ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ

Maana

Sema, "Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Waite mnao daia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu, hawamiliki uzito hata wa tembe hichi, katika Mbingu wala Ardhi, wala hawana ushirika wowote humo, wala yeye hana msaidizi miongoni mwao. [22]

[22] Ewe Nabii! Waambie washirikina: Waombeni hao mnao dai kwa uwongo kwamba ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, wakuleteeni manufaa au wakuondoleeni madhara. Hawakujibuni kitu. Kwani hao hawamiliki hata kiasi ya chembe ya kitu katika mbingu wala katika ardhi. Wala wao hawana ushirika wowote na Mwenyezi Mungu katika kuumba au kumiliki. Wala hapana yeyote katika hao miungu ya uwongo anaye msaidia Mwenyezi Mungu katika kupanga mambo ya viumbe vyake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, uwaambie washirikina, Waiteni wale ambao mlidai kuwa wao ni washirika wa Allah Mtukufu mkawaabudu badala Yake, miongoni mwa masanamu, malaika na binadamu, na wakusudieni katika haja zenu. Kwani wao hawatawaitika. Wao hawamiliki chochote, mbinguni wala ardhini, hata kadiri ya uzito wa mdudu chungu, na wala hawana ushirika katika hizo mbili. Na hakuna yoyote miongoni mwa hawa washirikina mwenye kumsaidia kuumba chochote. Bali Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, ndiye Aliyepwekeka kwa upatishaji.Yeye Ndiye Anayeabudiwa Peke Yake, na hakuna mwingine yoyote asiyekuwa Yeye anayestahiki kuabudiwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Saba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net