Saba 34:23
سبإوَلَا تَنفَعُ ٱلشَّفَـٰعَةُ عِندَهُۥٓ إِلَّا لِمَنْ أَذِنَ لَهُۥ ۚ حَتَّىٰٓ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمْ قَالُوا۟ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ ۖ قَالُوا۟ ٱلْحَقَّ ۖ وَهُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ
Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: "Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watasema: "Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipo kuwa kwa aliye mpa idhini. Hata itapo ondolewa khofu kwenye nyoyo zao watasema: Mola wenu Mlezi kasema nini? Watasema: Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa. [23]
[23] Wala maombezi kwa Mwenyezi Mungu hayawafai ila wenye kustahili makamo ya kuombewa. Mpaka itapo ondoka khofu katika nyoyo zao kwa kutolewa ruhusa ya kuombewa, hapo watakuwa wakiambiana kwa furaha: Mola wenu Mlezi kakwambieni nini? Na wengine watajibu kwamba alilo sema ni kauli ya haki, kwa kutoa ruhusa kuombewa aliye mridhi. Na Yeye peke yake, ndiye Mwenye Utukufu na Ukubwa. Na Yeye ndiye anaye ruhusu na kumkatalia amtakaye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na maombezi ya mwenye kuombea hayafai kitu na hayanufaishi mbele Yake, isipokuwa kwa yule Aliyemruhusu. Na miongoni mwa utukufu Wake, Aliyeshinda na kutukuka, ni kuwa Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anapotamka wahyi na watu wa mbinguni wakayasikia maneno Yake, wanakuwa katika hali ya kutetemeka kutokana na haiba yake, mpaka wanakuwa katika hali kama ile ya kukosa fahamu. Na kutetemeka kunapowaondokea kwenye nyoyo zao wanaulizana wao kwa wao, «Amesema nini Mola wenu?» Malaika watasema, «Amesema kweli! Na Yeye Yuko juu kwa dhati Yake, utendaji nguvu Wake na utukufu wa cheo Chake, Aliye Mkubwa juu ya kila kitu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net