Saba 34:24
سبإقُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ قُلِ ٱللَّهُ ۖ وَإِنَّآ أَوْ إِيَّاكُمْ لَعَلَىٰ هُدًى أَوْ فِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uongofu au upotovu ulio wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uwongofu au upotofu ulio wazi. [24]
[24] Ewe Nabii! Waambie washirikina: Nani anaye kuleteeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Watapo kuwa hawajibu kwa inda tu, waambie: Mwenyezi Mungu peke yake ndiye anaye kuruzukuni kutoka kote kuwili. Je! Ni sisi Waumini au nyinyi washirikina ndio walio katika moja ya hali mbili, ya uwongofu au upotofu ulio wazi?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Ni nani anayewaruzuku kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa mimea na madini na vinginevyo kutoka ardhini?» Hivyo basi hawana budi kukubali kuwa Yeye ni Allah Mtukufu. Na iwapo hawatakubali hilo, waambie, «Allah Mtukufu Ndiye Mwingi wa kuruzuku, na kwa hakika mojawapo wa mapote mawili, kati ya sisi na nyinyi, limejikita kwenye uongofu au limezama kwenye upotevu ulio wazi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net