Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 71

Al-Ahzaab 33:71

الأحزاب

يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَـٰلَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

Maana

Atawatengenezea vitendo vyenu na awasamehe madhambi yenu. Na anayemtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefuzu kufuzu kukubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa. [71]

[71] Apate kukuwezesheni kutenda mema, na azifute dhambi zenu. Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo amepata kufuzu kukubwa kwa kuepuka adhabu, na kupata thawabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mkimuogopa Allah Mtukufu na mkasema maneno ya sawa, Allah Mtukufu Atawasamehe dhambi zenu, Na mwenye kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake, katika kile alichokiamrisha na akakikataza, basi huyo amefaulu kupata utukufu mkubwa duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net