Al-Ahzaab 33:70
الأحزابيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَقُولُوا۟ قَوْلًا سَدِيدًا
Enyi mlioamini, mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa. [70]
[70] Enyi mlio amini! Iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu mkimuasi, na semeni maneno yalio simama sawa yasio kwenda upogo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo, fanyeni matendo ya kumtii na mjiepushe na matendo ya kumuasi, ili msistahili kupata mateso hayo. Na semeni, katika hali zenu zote na mambo yenu yote, maneno ya kunyooka na yanayolingana na usawa, yasiyokuwa na urongo na ubatilifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net