Al-Ahzaab 33:69
الأحزابيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ ءَاذَوْا۟ مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ ٱللَّهُ مِمَّا قَالُوا۟ ۚ وَكَانَ عِندَ ٱللَّهِ وَجِيهًا
Enyi mlioamini, msiwe kama wale waliomtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na hayo waliyoyasema, naye alikuwa mwenye heshima mbele ya Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio mtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na waliyo yasema, naye alikuwa mwenye hishima mbele ya Mwenyezi Mungu. [69]
[69] Enyi mlio amini! Msimuudhi Nabii kwa namna yoyote ya udhia, kama wale walio muudhi Musa katika kaumu yake. Na Mwenyezi Mungu akamtoa makosani na akamsafisha na hayo waliyo mzulia. Na Musa mbele ya Mwenyezi Mungu alikuwa ni bwana mwenye hadhi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, msimkere Mtume wa Allah Mtukufu kwa maneno wala kwa vitendo, wala msiwe mfano wa wale waliomkera Nabii wa Allah Mtukufu Mûsã, Allah Mtukufu Akamuepusha na kile walichokisema cha urongo na uzushi, na yeye alikuwa kwa Allah Mtukufu ni mwenye cheo kikubwa na utukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net