Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 68

Al-Ahzaab 33:68

الأحزاب

رَبَّنَآ ءَاتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ ٱلْعَذَابِ وَٱلْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا

Maana

Mola wetu Mlezi, wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa. [68]

[68] Mola wetu Mlezi! Wajaalie adhabu yao iwe mardufu, na uwafukuze kwenye rehema yako kabisa kwa kadri ya madhambi yao na makosa yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mola wetu! Waadhibu Motoni mara mbili zaidi ya adhabu unayotuadhibu kwayo, na uwafukuze kutoka kwenye rehema mafukuzo makali. Katika aya hii pana dalili ya kwamba kumtii asiyekuwa Allah Mtukufu katika kuenda kinyume na amri Yake na amri ya Mtume Wake, kunasababisha kupata hasira za Allah Mtukufu na mateso Yake, na kwamba mfuasi na mfuatwa watashirikiana kwenye adhabu. Basi ajihadhari na hilo Muislamu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net