Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 67

Al-Ahzaab 33:67

الأحزاب

وَقَالُوا۟ رَبَّنَآ إِنَّآ أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَآءَنَا فَأَضَلُّونَا ٱلسَّبِيلَا۠

Maana

Na watasema: "Mola wetu Mlezi, hakika sisi tuliwatii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio waliotupoteza njia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. [67]

[67] Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwafuata maraisi wetu, na wakubwa wetu katika kukukataa Wewe na Mtume wako. Na wao ndio wakatutenganisha mbali na Njia Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na watasema makafiri Siku ya Kiyama, «Mola wetu! Kwa kweli sisi tumewatii viongozi wetu katika upotevu na wakubwa wetu katika ushirikina wakatuepusha na njia ya uongofu na Imani».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net