Al-Ahzaab 33:72
الأحزابإِنَّا عَرَضْنَا ٱلْأَمَانَةَ عَلَى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱلْجِبَالِ فَأَبَيْنَ أَن يَحْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ مِنْهَا وَحَمَلَهَا ٱلْإِنسَـٰنُ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ ظَلُومًا جَهُولًا
Kwa hakika Sisi tuliwasilisha amana kwa mbingu na ardhi na milima, na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhalimu, mjinga.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga. [72]
[72] Sisi kwa hakika tulizitaka mbingu na ardhi na milima zichukue dhamana, nazo zikakataa kuichukua, na wakaiogopa. Lakini mwanaadamu aliichukua. Hakika yeye amekuwa ni mkubwa wa kujidhulumu nafsi yake kwa kutojua jukumu la kuchukua huko.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sisi tuliionyesha amana ambayo Allah Mtukufu Amewapatia waliokalifishwa na Sheria waitunze, nayo ni kufuata maamrisho na kujiepusha na makatazo kwa mbingu, ardhi na majabali, vikakataa kuibeba na vikaogopa visiweze kusimama kuitekeleza, na akaibeba binadamu na akashikamana nayo pamoja na udhaifu Wake. Hakika yeye ni mwingi wa udhalimu na ujinga wa nafsi yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net