Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 73

Al-Ahzaab 33:73

الأحزاب

لِّيُعَذِّبَ ٱللَّهُ ٱلْمُنَـٰفِقِينَ وَٱلْمُنَـٰفِقَـٰتِ وَٱلْمُشْرِكِينَ وَٱلْمُشْرِكَـٰتِ وَيَتُوبَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًۢا

Maana

Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake. Na awapokelee toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na anawapokelea toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [73]

[73] Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na Mwenyezi Mungu apate kukubali toba za Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwingi wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ili mwisho wa binadamu kuibeba amana uwe ni Allah Mtukufu kuwaadhibu wanafiki wa kiume wanaodhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri na wanafiki wa kike, na wanaume wanaomshirikisha katika ibada ya Allah Mtukufu asiyekuwa Yeye na wanawake washirikina, na ili Awakubalie toba Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwa kuzificha dhambi zao na kuacha kuwaadhibu. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa wenye kutubia miongoni mwa waja Wake, ni Mwenye huruma kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net