Saba 34:1
سبإٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَلَهُ ٱلْحَمْدُ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۚ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْخَبِيرُ
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote vilivyo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote viliomo mbnguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hikima, Mwenye khabari. [1]
[1] Sifa zote nzuri ni haki ya Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Mwenye kuumba, na Mwenye kumiliki, na Mwenye kupanga vyote vilioko mbinguni, na vilioko katika ardhi. Na Yeye peke yake ndiye Mwenye sifa Akhera, kwa kutamalaki kwake kuliko enea. Naye ndiye Mwenye hikima asiye kosa, Mwenye khabari zote, hapana asicho kijua siri yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Shukrani ni za Allah Mtukufu kwa sifa Zake ambazo zote ni sifa za ukamilifu, na kwa neema Zake za nje na za ndani za kidini na za kidunia, Ambaye Ana ufalme wa vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na ni Zake Yeye sifa njema zilizotimia huko Akhera, na Yeye Ndiye Mwenye hekima katika matendo Yake, Aliye Mtambuzi wa mambo ya viumbe Vyake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net