Al-Ahzaab 33:59
الأحزابيَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ قُل لِّأَزْوَٰجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَآءِ ٱلْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَـٰبِيبِهِنَّ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰٓ أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Ewe Nabii, waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana kwa hivyo wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. [59]
[59] Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake wa Waumini, wateremshe nguo zao juu ya miili yao. Na wakivaa namna hii ni afadhali na wanaelekea zaidi kujuulikana na kwa hivyo wasipate kuudhiwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kumrehemu mwenye kuacha madhambi yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Waambie wake zako, watoto wako wa kike na wanawake Waumini wateremshe juu ya vichwa vyao na nyuso zao mashuka yao na mitandio yao, ili kufinika nyuso zao, vifua vyao na vichwa vyao. Kufanya hivyo kuko karibu zaidi kuwafanya wao watenganishwe kwa kusitirika na kuhifadhika, wasiwe ni wenye kusumbuliwa kwa kukerwa wala kuudhiwa. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe na kurehemu kwa kuwa Amewasamehe yaliyopita na Akawarehemu kwa kuwabainishia halali na haramu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net