Al-Ahzaab 33:60
الأحزابلَّئِن لَّمْ يَنتَهِ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْمُرْجِفُونَ فِى ٱلْمَدِينَةِ لَنُغْرِيَنَّكَ بِهِمْ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَآ إِلَّا قَلِيلًا
Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitina katika Madina hawataacha, basi kwa yakini tutakupa mamlaka juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako isipokuwa muda mchache tu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu. [60]
[60] Ninaapa! Ikiwa hawataacha hao wanaafiki, na wenye maradhi katika nyoyo zao, na wanao eneza khabari za uwongo katika Madina, hapana shaka nitakusalitisha juu yao, kisha hawatabakia kuwa karibu yako ila kwa muda mchache tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wasipokomeka, wale wanaoficha ukafiri na kudhihirisha Imani, wale ambao ndani ya nyoyo zao mna shaka na wasiwasi na wale wanaoeneza habari za urongo katika mji wa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na mabaya yao na shari zao, tutakupa uwezo juu yao, kisha hawatakaa pamoja na wewe humo isipokuwa muda mchache.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net