Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 33 · Aya ya 58

Al-Ahzaab 33:58

الأحزاب

وَٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ بِغَيْرِ مَا ٱكْتَسَبُوا۟ فَقَدِ ٱحْتَمَلُوا۟ بُهْتَـٰنًا وَإِثْمًا مُّبِينًا

Maana

Na wale wanaowaudhi Waumini wanaume na wanawake pasi na wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhuluma kubwa na dhambi iliyo dhahiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri. [58]

[58] Na wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake kwa maneno au vitendo, bila ya wao kufanya makosa yoyote, hao basi wamebeba migongoni mwao mzigo wa ule uwongo wao, na inakuwa wametenda dhambi iliyo dhaahiri ubaya wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wenye kuwaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwa maneno au vitendo bila ya kosa walilolifanya, basi watakuwa wametenda tendo la urongo na uzushi mbaya kabisa, na wamefanya kosa chafu waziwazi, ambalo kwalo watastahili kupewa adhabu huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Ahzaab

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net