Al-Ahzaab 33:57
الأحزابإِنَّ ٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا مُّهِينًا
Hakika wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi. [57]
[57] Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuwapinga na kuchochea watu wawakatae, Mwenyezi Mungu amewafukuza kwenye rehema yake duniani na Akhera; na amewaandalia adhabu itayo wavunja kiburi chao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale wanaomuudhi Allah Mtukufu kwa kumshirikisha na kufanya maasia mengine, na wakamuudhi Mtume wa Allah Mtukufu kwa maneno na vitendo, Allah Mtukufu atawafukuza na Atawaweka mbali na kheri duniani na Akhera, na Amewaandalia, huko Akhera, adhabu kali yenye kuwadhalilisha na kuwafanya wanyonge.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net