Al-Ahzaab 33:56
الأحزابإِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَـٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِىِّ ۚ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ صَلُّوا۟ عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا۟ تَسْلِيمًا
Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi mlioamini, mswalieni na mumsalimu kwa salamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu. [56]
[56] Hakika Mwenyezi Mungu anamrehemu Nabii wake na yu radhi naye. Na Malaika wanamwombea yeye. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Anamsifu Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), mbele ya Malaika waliokurubishwa. Na Malaika Wake wanamsifu Nabii na wanamuombea Allah Mtukufu, basi enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, mswalieni Mtume wa Allah Mtukufu na mtakieni amani, kwa kumuamkia na kumtukuza. Na namna ya kumswalia Nabii, (rehema na amani zimshukie), imethibiti kwenye Sunnah kwa aina mabalimbali, miongoni mwazo ni: «Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na watu wa Muhammad, kama ulivyowarehemu watu wa Ibrãhîm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa ni Mwingi wa kutukuzwa. Ewe Mola! Mbariki Muhammad na watu wa Muhammad kama ulivyowabariki watu wa Ibrãhîm, hakika wewe ni Mwingi wa kushukuriwa, ni Mwingi wa kutukuzwa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net